Orkonerei FM

Afisa Kilimo Simanjiro Awataka Wakulima Kufuata Misingi Bora ya Kilimo Ili Kupata Mavuno Mengi

28 August 2026, 3:32 pm

picha kwa msaada wa mtandao

Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Simanjiro, Jenifar Mbuya, amewataka wakulima mkoani humo kufuata kanuni na misingi bora ya kilimo ili kujiwekea mazingira ya kupata mavuno mengi na yenye tija.

Na Dorcas Charles

Akizungumza na Mwandishi wetu Dorcas Charles amesema taratibu sahihi za uandaaji wa mashamba na upandaji, Afisa Kilimo huyo ameeleza kuwa ili mpeto au mavuno ya mkulima yawe yenye tija, mkulima anapaswa kuandaa shamba lake mapema kwa kutumia trekta na kufuata kanuni sahihi za upandaji badala ya kutumia njia zisizo rasmi.

Makosa Yanayopunguza Mavuno Mashambani

Afisa Mbuya amebainisha kuwa wakulima wengi wamekuwa wakifanya makosa wakati wa upandaji kwa kufuatisha mbegu nyuma ya trekta badala ya kutumia jembe la mkono au kifaa maalum cha kupandia (planter).

Kulingana na maelezo yake, kufuata trekta wakati wa kupanda kunasababisha changamoto zifuatazo:

  • Ubali mkubwa kati ya mistari: Inasababisha nafasi kati ya jembe na jembe kufika mpaka sentimita 90, badala ya sentimita 60 hadi 70 zinazotakiwa kwa mbegu nyingi za mahindi.
  • Mtawanyiko mbaya wa mbegu: Mbegu zingine huangukia sehemu yenye udongo mwingi uliopitiliza au kutositiriwa vyema na udongo, jambo linalofanya zishindwe kuota vizuri.
  • Kupungua kwa kiwango cha mbegu: Badala ya kupanda kilo 8 hadi 10 za mbegu kwa heka moja, wakulima wengi wanaofuata trekta huishia kupanda kilo 5 hadi 6 pekee, jambo linalopunguza idadi ya mimea na kuleta mavuno kidogo.
  • Mshindano wa lishe: Mbegu zinapojikusanya sehemu moja, mimea inakuwa na ushindani wa chakula na kusababisha kustawi ikiwa dhaifu.