Orkonerei FM

Ulemavu Sio Kikwazo cha Uongozi Naisinyai

14 September 2026, 11:54 am

Picha inamuonyesha Bwana Supeti mwenyekiti wa watu wenye ulemavu Naisinyai akizungumza na mwandishi wetu Isack Dickson, Picha Na Dorcas Charles;

“Nimejitokeza kwa sababu najiamini. Watu waliona uwezo ndani yangu na ndio maana wakanichagua,”

Na Isack Dickson

Katika Kijiji cha Losoito, Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara yupo kijana mmoja mwenye msimamo, uthubutu na ndoto kubwa ya kuwa sauti na mwakilishi wa kundi la watu wenye ulemavu. Kijana huyu si mwingine bali ni Supeti, Mwenyekiti wa Watu Wenye Ulemavu Kata ya Naisinyai, ambaye pia anahudumu kama Katibu Hamasa wa Vijana katika Kijiji cha Anachotoka.

Licha ya kushika nafasi hizo za uongozi, Supeti anakabiliana na changamoto mbalimbali katika maisha yake ya kila siku, ikiwemo kuwa mlemavu pekee anayejitokeza kimasomo na kijamii katika eneo lake, pamoja na changamoto kubwa ya usafiri kutoka anapokaa hadi kufika tawi la Losoito.

Habari hii inatukumbusha kuwa kama jamii, tuna jukumu la kuhakikisha mazingira yanakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu—sio kwa kuwahurumia, bali kwa kuwapa haki na fursa zao za msingi.

Karibu kusikiliza stori hii inayosimuliwa na mwandishi wetu Isack Dickson.

Sauti ya mahojiano ya Isack Dickson akizungumza na Bwana Supeti mwenyekiti wa watu wenye ulemavu Naisinyai pamoja na wananchi wa kata hyo.