Orkonerei FM

Jinsi Ukame Unavyotishia Maisha ya Wahadzabe na Wadatoga Karatu

12 September 2026, 6:13 pm

Navaya Ndaskoi kutoka shirika la PINGOs Forum akieleza namna mabadiliko ya tabianchi na matumizi ya ardhi yanavyoathiri maisha ya Wahadzabe na Wadatoga.
📸: Isack Dickson

Katika maeneo yanayozunguka Ziwa Eyasi wilayani Karatu, mabadiliko ya tabianchi na ukame vimegeuka kuwa mtihani mzito wa kila siku kwa jamii za asili za Wahadzabe na Wadatoga. Mbali na wanawake kutembea saa kadhaa au kununua dumu la maji kwa shilingi 1,000, wafugaji wanashuhudia mifugo yao ikifa kutokana na kukauka kwa vyanzo vya maji na kupungua kwa malisho.

Na Isack Dickson

Ukame unaoendelea kushika kasi katika eneo la Ziwa Eyasi umezidisha ugumu wa maisha,wanawake kama Halima Sabena wa jamii ya Wahdzabe wanalazimika kununua dumu la maji la lita 20 kwa shilingi 1,000 au kutembea umbali mrefu, huku akina mama wa Kidatoga kama Dede wakilazimika kufukua mchanga kando ya mto Mto Baray ili kupata maji yanayochuruzika kwa shida.

Athari hizi hazijaishia kwa akina mama pekee; wafugaji wa jamii ya datoga wanapoteza mamia ya mifugo kutokana na ukosefu wa malisho na maji, huku mabadiliko ya matumizi ya ardhi yakibana zaidi maeneo yao ya asili.

Katika makala hii ya sauti iliyotayarishwa na Isack Dickson, tunasikia sauti za wanajamii wakieleza hofu yao juu ya mustakabali wa watoto wao, uchambuzi kutoka kwa Navaya Ndaskoi wa shirika la PINGOs Forum, pamoja na majibu ya Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Dr. Lameck Karani, kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali kulinda maeneo na rasilimali za jamii hizi.

Makala ya Sauti (Kiswahili)