Orkonerei FM
Orkonerei FM
15 November 2026, 3:09 pm

picha ya mkuu wa shule ya sekondari Terrat Mwl.Julius Maplani akizungumza na wazazi pamoja na wananfunzi. (picha na Isack Dickson)
Kusubiri vijana wafikie umri wa ukomavu wa kiakili kabla ya kuwapeleka kwenye mila za tohara ni hatua muhimu inayoweza kusaidia kulinda nidhamu, kuongeza ufaulu na kuhifadhi heshima ya tamaduni katika jamii.
Na Isack Dickson
Wazazi na walezi katika Kata ya Terrat, Wilaya ya Simanjiro, wametakiwa kuacha kuwapeleka watoto wadogo kwenye mila za tohara kabla ya kukamilisha elimu yao ili kulinda uwezo wao wa kifikra na maadili wanapokuwa shuleni.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa shule ya Sekondari Terrat Wilaya ya Simanjiro Mwl.Julius Maplani Novemba 13 ,2026 katika mahafali ya 17 ya kidato Cha nne yaliyofanyika shuleni hapo ambapo alibainisha kuwa watoto wanaokimbizwa kwenye mila wakiwa wadogo hutafsiri ujasiri vibaya na kushindwa kuhimili misingi ya masomo.
Aidha, amewapongeza wazazi waliosimamia elimu ya vijana wao hadi wakamaliza kidato cha nne bila kukatisha masomo, akisisitiza kuwa hatua hiyo inawapa nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa kimaisha.
sauti ya mkuu wa shule ya sekondari Terrat.

picha inawaonyesha wazazi na baadhi ya wanafunzi walioitimu kidato cha nne shule ya sekondari Terrat. (picha na Isack Dickson)