Orkonerei FM

Wakulima Terrat watakiwa kujiandaa mapema

17 September 2026, 5:47 pm

Picha ya afisa kilimo kata ya Terrat bwana Juma Thabiti akizungumza na mwandishi wetu Dorcas Charles. (picha na Isack Dickson)

Matumizi ya mbegu bora, pamoja na maandalizi sahihi ya mashamba kwa wakati, ni miongoni mwa hatua muhimu zinazoweza kusaidia kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.

Na Dorcas Charles

Wakulima katika Kata ya Terrat, Wilaya ya Simanjiro, wametakiwa kuanza mapema maandalizi ya mashamba yao kwa ajili ya msimu ujao wa kilimo ili kupata muda wa kutosha wa kujiandaa kabla ya msimu wa upandaji kuanza.

Wito huo umetolewa na Afisa Kilimo wa Kata ya Terrat, Juma Thabiti, wakati akizungumza na Orkonerei FM Radio, ambapo amesisitiza kuwa maandalizi ya mapema ni muhimu katika kuhakikisha wakulima wanapata msimu wenye tija.

Aidha, Thabiti amewataka wakulima kutumia mbegu bora zilizothibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) ili kuongeza uwezekano wa kupata mavuno bora.

Sauti ya fisa kilimo kata ya Terrat bwana Juma Thabiti.

Kwa undani zaidi kuhusu maandalizi ya msimu wa kilimo, wananchi wanahimizwa kusikiliza Kurunzi Maalum, kesho saa 2:30 asubuhi, kupitia Orkonerei FM Radio.