Orkonerei FM

Jamii yashauriwa kutumia mifuko ya ‘kinga njaa’ kuhifadhi chakula salama

26 August 2026, 11:49 am

Picha ya mifuko ya Kinga Njaa ikiwa na bidhaa.

Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro imewataka wananchi na wakulima wilayani humo kutumia njia salama na zilizothibitishwa katika kuhifadhi mazao ya chakula, hususan yale yanayotengwa kwa ajili ya matumizi ya familia, ili kuepuka madhara ya kiafya yanayoweza kusababishwa na matumizi yasiyo sahihi ya kemikali.

Na Dorcas Charles

Wito huo umetolewa umetolea na Afisa Kilimo kutoka halmashauri ya Simanjio Nenifa Mbuya, huku wananchi wakishauriwa kutumia vifungashio salama visivyo na kemikali, pamoja na mapipa na viuatilifu vilivyothibitishwa kwa ajili ya kuhifadhi mazao kwa muda mrefu.

Kwa wale wanaohifadhi mazao kwa kiwango kikubwa kwenye maghala, wataalamu hao wameshauri matumizi ya viuatilifu vilivyothibitishwa, hususan vya unga, ili kulinda akiba hiyo kwa muda mrefu. Elimu hiyo inalenga kuongeza usalama wa chakula kuanzia ngazi ya familia hadi kwenye maghala makubwa ya kibiashara na kuhakikisha afya ya mlaji inalindwa wakati wote.

Sauti ya Afisa Kilimo kutoka halmashauri ya Simanjio Nenifa Mbuya