Orkonerei FM
Orkonerei FM
27 August 2026, 1:13 pm

Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma (DHO) Wilaya ya Simanjiro, Ghati Megewa, akiwa studio za Orkonerei Fm Radio (Picha na Isack Dickson)
Katika kuunga mkono juhudi za serikali za kulinda afya za watoto nchini, Wilaya ya Simanjiro imekamilisha maandalizi ya utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya polio inayowalenga watoto wote kuanzia umri wa miezi sifuri hadi miaka tisa.
Na Joyce Elius
Akizungumzia utekelezaji wa kampeni hiyo katika wilaya hiyo kuanzia Agosti 27 hadi Agosti 30, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma na Huduma za Afya Ngazi ya Jamii Wilaya ya Simanjiro, Gati Megewa, ameeleza kuwa chanjo hiyo inatolewa bila gharama katika vituo vyote vya afya, zahanati, na hospitali wilayani humo kupitia idara ya huduma za mama na mtoto.
Megewa amefafanua kuwa kampeni hii ya kitaifa imekuja kufuatia hatua za tahadhari baada ya kirusi cha polio aina ya pili (Type 2) kugundulika kwenye sampuli za maji mkoani Mwanza mwaka jana (2025), ingawa Tanzania ilitangazwa kutokuwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2016.
Sauti ya Megewa