Orkonerei FM

Manyara watakiwa kujipanga kuepuka madhara ya El Nino

1 September 2026, 12:37 pm

Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Mkoa wa Manyara, Bi. Salma Amour Suleiman.

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Mkoa wa Manyara imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu msimu wa mvua za Vuli zinazotarajiwa kuambatana na hali ya El Nino. Mamlaka imeonya kuwa mvua hizo zitakuwa nyingi zaidi ya wastani wa kawaida na zinaweza kusababisha madhara makubwa endapo hatua madhubuti hazitachukuliwa mapema.

Na Isack Dickson

Akizungumza kuhusu mwelekeo wa msimu huu, kwa njia yya simu, Meneja wa TMA Mkoa wa Manyara, Bi. Salma Amour Suleiman, amesisitiza kuwa uwepo wa hali ya El Nino unamaanisha ongezeko kubwa la mvua, hivyo kila mwananchi kuanzia ngazi ya kaya hadi kwenye sekta za uzalishaji anapaswa kujiandaa kikamilifu.

Sauti ya Meneja wa TMA Mkoa wa Manyara