Orkonerei FM
Orkonerei FM
21 September 2026, 4:48 pm

Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mwalimu Fakii Lulandala, ameeleza hatua zilizochukuliwa na Kamati za Usalama na Maafa kukabiliana na mvua za El Niño, ikiwemo kuwataka wakazi wa maeneo hatarishi kuhama mapema.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mwalimu Fakii Lulandala, ameeleza hatua zilizochukuliwa na Kamati za Usalama na Maafa kukabiliana na mvua za El Niño, ikiwemo kuwataka wakazi wa maeneo hatarishi kuhama mapema.
Wilaya ya Simanjiro imetangaza mikakati madhubuti ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Niño, kupitia vikao vilivyofanywa na Kamati ya Usalama na Kamati ya Maafa ya Wilaya.
Mwl.Lulandala amesema vijiji vya Kilombero, Nakweni, Shambarai, na Olbili vipo katika hatari kubwa ya kufungwa kwa barabara na kutofikika. Kutokana na tishio hilo, Halmashauri imeagizwa kujiandaa na vifaa vya dharura ili kuwezesha huduma kufika kwenye vijiji hivyo endapo barabara zitakatika.
Mkuu wa Mkoa pia anatarajiwa kufanya ziara ya kukagua maeneo hatarishi zaidi na kutoa maelekezo yatakayosaidia kunusuru uwezekano wa makao makuu ya wilaya na maeneo mengine kutofikika kiurahisi.
Mkuu wa Wilaya amehitimisha kwa kusisitiza kuwa kila mwananchi ni mlinzi namba moja wa usalama wake na wa jirani yake, huku akiwaomba viongozi wa madhehebu ya dini kuendelea kumuomba Mungu ili majanga haya yasiwe makubwa kama inavyohofiwa.