Orkonerei FM
Orkonerei FM
24 August 2026, 11:15 am

Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro inatarajia kuwafikia watoto 116,152 chini ya umri wa miaka 10 kwenye Kampeni Maalum ya Chanjo ya Polio itakayofanyika kwa awamu mbili kuanzia mwezi huu wa Agosti.
Na Dorcas Charles
Mkoa wa Manyara, kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, uko katika maandalizi kabambe ya kuendesha Kampeni Maalum ya Chanjo ya Polio inayolenga kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa huo unaosababisha kupooza.
Katika mahojiano maalum, Ghati Megewa, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma na Afya ya Jamii kutoka Ofisi ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, anaeleza kuwa kampeni hiyo itafanyika kwa awamu mbili na inatarajia kuwafikia jumla ya watoto 116,152 wilayani humo.
Ratiba ya Kampeni:

Naye Mzee wa Kimila kutoka Terrat, Simanjiro, Bwana Godson Nduya Lukumay, ametoa wito kwa jamii, wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wahudumu wa afya watakaopita nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha kila mtoto anayestahili anapata chanjo hiyo salama.