Orkonerei FM
Orkonerei FM
20 August 2026, 1:50 pm

Na Isack Dickson
Mkoani Manyara, maandalizi yamekamilika kuelekea kampeni ya chanjo ya matone ya Polio itakayofanyika Agosti 27 hadi 30, 2026. Watoto 675,630 walio chini ya umri wa miaka 10 wanatarajiwa kufikiwa na chanjo hiyo. Wanahabari wamepewa elimu ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wazazi na walezi kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo. Sikiliza Simulizi hapa chini..