Orkonerei FM

Tahadhari za TMA zinafika kwa wafugaji,na ipi nafasi ya maarifa ya asili?

17 June 2026, 2:25 pm

Viongozi wa jamii ya kimasai wakitoa baraka kwa watoto ,wazee katika jamii hii wanatumika kwa shuhuli mbalimbali haswa kutokana na maarifa waliyonayo ikiwamo baraka,utabiri na kutatua migogoro. (Picha kwa Msaada wa Mtandao)

TMA imetoa utabiri wa msimu wa kipupwe wa mwaka 2026, ikiwataka wafugaji kujiandaa na baridi, upepo, upungufu wa maji na malisho. Lakini je, taarifa hizi zinawafikia wafugaji wa Kimasai wa kwa wakati na kuwasaidia kufanya maamuzi ya kulinda mifugo yao? na nafasi ya tabiri za kutumia maarifa ya asili ni ipi?

N a Isack Dickson

Makala hii inafuatilia safari ya taarifa za hali ya hewa kutoka kwa mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa (TMA) hadi kwa wafugaji. Inachunguza namna wafugaji wanavyopata na kutumia utabiri wa kisasa, nafasi ya maarifa ya jadi, changamoto za upatikanaji wa taarifa na namna mabadiliko ya tabianchi yanavyozidisha umuhimu wa tahadhari za mapema katika kulinda mifugo, maji na malisho.

Makala kamili ya sauti.