Kitulo FM
Kitulo FM
5 October 2026, 8:09 pm

baadhi ya wananchi wakiwa katika zoezi la kuzibua mitaro ya maji
kutokana na mamlaka ya hali ya hewa nchini Tanzania kutoa taarifa za ujio wa mvua za eli nino wananchi wameendela na zaezi la kuzibua mitaro ya maji pamoja na kukata miti iliyo pembezoni mwa barabara pamoja na kukumbushana namna ya kujikinga na mvua hizo ili zisije kuleta madhara makubwa
na Rose njinile.
Katika kuhakikisha tahadhari ya mvua za el nino zinaendelea kuchukuliwa , wananchi wa ivalalila na mwongolo hii leo oktoba 5,2026 wamejitokeza katika zoezi la kuzibua mifereji inayopitisha maji pamoja na kukata miti iliyo pembezoni mwa barabara
Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa ndg Joseph Mbilinyi ameungana na wananchi wa mwongolo na ivalalila katika zaezi hilo la kuzibua mitaro hiyo ya maji huku akiwapongeza wananchi kwa umoja wao wakujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ambalo ni njia moja wapo ya kuchukua tahadhari ya mvua hizo
sauti ya joseph mbilinyi 01
Mwenyekiti wa muungano ivalalila ndg Lazaro Chaula amewasii wananchi wa ivalalila kutokana na mvua hizo zinazotarajiwa kuanza kunyesha mwezi huu Kuendela kuchukua tahadhari pamoja na kuweka akiba ya chakula huku akimpongeza mkuu wa wilaya ya makete mhe kissa Gwakisa kasongwa kwa kuendelea kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari ya mvua hizo
sauti ya mwenyekiti wa muungano Lazaro 02

zaezi la kuzibua mifereji likiendela kwa wananchi
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha ikiligano ndg Noad Mbilinyi amesema kuwa wao kama viongozi wamekuwa wakiendelea kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi katika ameneo hatarijishi kuweza kuchukua tahadghari ya mvua za el nino zinazotarajia kunyesha kuanzia mwezi huu wa oktoba
sauti ya Noad Mbilinyi 03
Nao baadhi ya wananchi wa ivalalila na mwongolo akiwemo Gwido Mahenge,Elizabeti chaula wameshukuru kwa zoezi hilo lililofanyika hukuwakiwapongeza viongozi wao kwa kuendela kutoa elimu kuhusu mvua hizo za eli nino
sauti ya wananchi 04