Kitulo FM

Mbunge Sanga akabidhi baiskeli kwa mlemavu Makete

November 1, 2023, 1:19 pm

Mwonekanao wa baiskeli iliyokabidhiwa kwa mlemavu wa kijiji cha Kisinga Sinahabari. Picha na mwandishi wetu

baada ya wananchi wa kijiji cha kisinga kupaza sauti dhidi ya mlemavu Sinahabari mbunge wa jimbo la makete Festo Sanga kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wamemkabidhi baiskeli yenye thamani ya shilingi milioni moja

Na Ahazi Ndelwa.

Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe Mhe. Festo Sanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliopo kijiji cha Kisinga na nje ya kijiji hicho wamefanikisha kununua baiskeli ya mlemavu aitwaye Sinahabari yenye thamani ya shilingi milioni moja.

Makabidhiano ya baiskeli hiyo yamefanyika kijiji cha Kisinga kata ya Lupalilo wilayani Makete kwa niaba ya mbunge na wadau wakiwakilishwa na diwani wa kata hiyo Mhe. Imani Mahenge tarehe 29 Oktoba 2023.

Mhe. Mahenge amemshukuru mbunge, wadau na Redio Kitulo FM kwa namna ambavyo wamekuwa na mchango mkubwa katika kufanikisha jambo hilo na kumsaidia mlemavu huyo wa viungo.

Kwa niaba ya Watangazaji wa Kitulo FM waliowakilishwa na Ahazi Ndelwa, amesema Redio imekuwa na mchango mkubwa wa kutafuta walemavu wanaoshindwa kupata mahitaji muhimu na kutafuta wadau ili waweze kuchangia baadhi ya mahitaji ikiwemo ununuzi wa Baiskeli za magurudumu matatu