Waziri Mhe.Balozi Dkt. Pindi Chana akabidhi bati 200 Iwawa Sekondari
Kitulo FM

Waziri Pindi Chana akabidhi Bati 200 Iwawa Sekondari

July 4, 2023, 8:17 am

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amekabidhi Bati 200 shule ya Sekondari Iwawa zenye thamani Zaidi ya Milioni 8 kwa ajili ya kuezeka Bweni la Wavulana kidato cha tano na sita.

Akibabidhi bati hizo zilizotolewa na wadau wa Bank ya NMB amesema Serikali inatambua jitihda kubwa zinazofanywa na Bank hiyo ikiwemo kusaidia uboreshaji wa miundombinu ya Elimu.

Katika makabidhiano hayo alikuwepo Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Makete Ndg. Clement Ngajilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Hawa Kader, Augustino Ngailo Afisa Tarafa Lupalilo (kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya), Jackline Mrosso Kaimu Mkurugenzi Mtendaji (W) ya Makete, Mhe. Francis Chaula Diwani Kata ya Iwawa pamoja na baadhi ya Madiwani na wananchi.

Wille Mponzi Meneja NMB Kanda ya Nyanda za Juu kusini amesema wao kama wadau wa Maendeleo wataendelea kusaidia shughuli mbalimbali upande wa elimu ili kuunga mkono jitihada za Serikali.