Merry Cahatanda atembelea Makete na kuzungumza na Wananchi Kigala
Kitulo FM

Chatanda: Changamoto ya barabara Kigala-Makete nitaifikisha kwa waziri

July 5, 2023, 7:11 am

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) UWT Marry Chatanda amesema kilio cha mbunge na wananchi wa Kigala kuhusu barabara atakifikisha kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.

Chatanda amesema hayo akiwa na wananchi wa Kigala kwenye mkutano wa hadhara aliofanya Julai 4, 2023 kijijini hapo na kusikiliza changamoto kubwa inayowakabili wananchi wa Kigala ambayo ni barabara yenye urefu wa Km. 17 kutoka Matenga kata ya Ikuwo.

“Nimesikia kilio chenu kutoka kwenu na kwa mbunge wenu Mhe. Sanga, namfahamu sana mbunge wenu na anajua kuipigania Makete na barabara ya Ikuwo-Nkenja ameisemea sana bungeni, habari njema ni kwamba tayari Mhe. Rais ameipandisha hadhi kuwa ya TANROAD ili ihudumiwe kwa ukubwa wake”

“Lakini Mhe. Rais anawapenda na kwa kuwa ameibeba barabara hii kubwa niseme kipande cha Kilomita 17 hizi kutoka Ikuwo kuja hapa Kigala nitaongea na Waziri anayehusika na kwa kuwa Mhe. Mbunge ni mfuatiliaji tusaidiana kuhakikisha wananchi wa Kigala mnatengenezewa Barabara hii”

Mbunge wa Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kigala amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipandiba hadhi barabara ya Mfumbi, Ikuwo-Nkenja, kutoa fedha za ukamilishaji wa Zahanati Kigala, Ujenzi wa mnara wa Mawasiliano ambapo wananchi hao hawakuwa na mawasiliano kabisa.

“Niwaambie tu kwamba kazi kubwa inafanywa na Mhe. Rais anafanya kwenye Wilaya Makete lakini katika Kata hii ametoa fedha nyingi sana na tunaomba ukatufikishie salamu na shukrani zetu kwakena kumuomba aweze kuwasaidia wananchi kutatua Changamoto ya Barabara”

Wananchi wa Kijiji cha Kigala wameishukuru Serikali kwa fedha ilizotoa kwa ajili ya Maendeleo kijijini hapo na kuiomba Serikali iweze kuwasaidia changamoto kubwa ya Barabara ya Matenga-Mlengu mpaka Kigala