Kitulo FM

Fedha zatolewa na serikali ujenzi wa nyumba za walimu Makete

September 29, 2023, 9:04 am

kamati ya siasa mkoa wa Njombe.picha na Furahisha Nundu

Ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa shule ya Makete ilitopo katika kata ya Mlondwe wilayani Makete serkali imeendelea kutoa fedha kwaajili ya kukamilisha Ujenzi wa Miundombinu ya shule hiyo

na Furahisha Nundu

Kiasi cha shilingi milioni  100 kimetolewa na serikali kujenga nyumba ya walimu katika shule ya sekondari Makete iliyopo kata ya Mlondwe.

Kamati ya siasa mkoa wa Njombe imefika shuleni hapo  kukagua ujenzi wanyumba hiyo  huku ikiipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha  mazingira ya shule hiyo mpya iliyoanza mapema mwaka huu.

Katika ziara ya ukaguzi wa shule hiyo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Mhe:Deo sanga (MB) ameongozana na wanakamati wengine akiwemo Clement Ngaji mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete,MH:Festo Sanga (MB) na diwani wa kata ya Mlondwe Mh:Alfonc Salimo pamoja na wataalamu kutoka H/W

Kwaupande wake Diwani wa kata ya Mlondwe Mh:Alfonce Salimo kwa niaba ya wananchi wa Mlondwe ameiomba serikali kukarabati barabara ya kutoka Kijiji cha Mbela mpaka Makete sekondari kwakua kipindi cha masika miundombinu ya barabara imekua changamoto na kupelekea kukwamisha juhudi za maendeleo  hususani kufikisha vifaa shulen hapo.

Mbunge jimbo la makete Mhe.Festo Sanga ameshukuru serikali kwa kutenga fedha zaidi ya milioni 500 kujenga shule ya sekondari ya Makete ambayo itakwenda kuondoa changamoto ya wanafunzi kwenda shule ya sekondari Mlondwe,

wananchi wakiwa kwenye mkutano wa kamati ya siasa Mlondwe.picha na Furahisha Nundu