Kitulo FM

Wazazi wahimizwa kutoa michango shuleni

4 June 2026, 9:41 am

Wananchi pamoja na viongozi wakiwa kwenye mkutano wa kijiji

Kutokana na kukubaliana kwenye vikao shuleni, wazazi wamewaasa wenzao wasiotoa michango pamoja na kuwatumia watoto wao kwenye utafutaji kuacha tabia hiyo.

Na Mwandishi Wetu

Wazazi pamoja na viongozi wa kijiji cha ivalalila kata ya iwawa wilaya ya makete  wamesikitishwa na baadhi ya wazazi na walezi kushindwa kutoa michango ya  shule baada ya kukubaliana katika mikutano

Hayo yamejiri hii leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha ivalalila kata ya iwawa ambapo umehudhuriwa pia na mwenyekiti wa halmashauri ambaye pia  ni diwani wa kata ya iwawa mhe Rabson mahenge pamoja na mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdg wa iwawa ndg Joseph mbilinyi

Wananchi kijiji cha Ivalalila wakiwa kwenye mkutano

Diwani wa kata ya iwawa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya makete mhe Rabson Mahenge amewasii wazazi na walezi kutokufanya masihara kwenye swala la elimu na badala yake wajivunie kuwasomesha watoto wao kwamanufaa ya kwao na taifa kwa ujumla

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri Mhe Rabson Mahenge

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete na Diwani wa kata ya Iwawa Rabson Mahenge

Akizungumza mwalimu mkuu wa shule ya msingi ivalalila mwl Amina Kyando amekili kuwa na watoto ambao  ni wasumbufu na watoro katika shule hiyo huku akieleza njia ambayo ametumia kwa baadhi ya wanafunzi watoro ili wasiweze kurudia jambo hilo

Sauti ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwl Kyando

NAO baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo akiwemo jimines mahenge mkutano huo wamewasisitiza wazazi kuacha kuwaingiza watoto wao katika shughuli za utafutaji jambo ambalo limekuwa likisababisha utoro pamoja na watoto kushindwa kufanya vyema mitihani yao

Sauti ya wananchi wa kijiji cha Ivalalila
Wakazi wa kijiji cha Ivalalila wakiendelea kuchangia hoja zilizowasilishwa na viongozi

Wakati huo huo diwani mahenge ameahidi kutoa kumpyuta katika shule ya msingi ivalalila itakayo wasidia walimu katika majukumu yao ya kazi ya kila siku

Sauti ya Diwani Mahenge kuhusu kopyuta

Nae mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdg wa iwawa ndg joseph mbilinyi  amewasiii wananchi wa ivalalila kuendelea kuwaheshimu viongozi waliowachagua pamoja na wataalAmu ambao serikali imewaletea

Sauti ya wenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Iwawa