Zoezi la upimaji urefu kwa watoto likiendelea
Kitulo FM

Ushauri: Zingatieni lishe bora kwa watoto

June 23, 2023, 8:10 am

Wazazi na walezi kijiji cha Ihela Kata ya Tandala wilayani Makete wamekumbushwa namna ya kuzingatia lishe bora kwa watoto ili kuhakikisha wanakuwa na Afya imara.

Akizungumza na Wazazi na walezi wa kijiji hicho tarehe 21 Juni, 2023 Bi. Jackline Nanauka Afisa Lishe Wilaya ya Makete akiwa kwenye Maadhimisho ya siku ya Lishe amesema lishe ndio msingi wa Afya bora kwa watoto hivyo Wazazi wanapaswa kuhakikisha elimu wanayoipata kutoka kwa wataalamu kuhusu Lishe bora wanazingatia ipasavyo.

Vilevile siku hiyo imeambatana na utoaji wa matone ya Vitamini A, upimaji wa watoto (Uzito, urefu na hali ya Lishe) pamoja na chanjo kwa watoto