Mkurugenzi wa TARI MLINGANO Tanga DKT. Catherine Senkoro akiwa na Mwandishi wa Kitulo FM kwenye shamba la Mfano la Ngano Kigala iliyotolewa na ASA
Kitulo FM

Maadhimisho Siku ya Mkulima yafanyika Makete

June 21, 2023, 7:58 am

Tarehe 16 Juni kila mwaka hufanyika maadhimisho ya Siku ya Mkulima, ambapo katika wilaya ya Makete yamefanyikia kijiji cha Kigala kwenye mashamba ya mfano ya ngano.

Katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na wakulima, mkurugenzi wa TARI Mlingano na ASA mgeni rasmi alikuwa afisa tarafa ya Ikuwo Alberto Luondo.

Serikali kupitia taasisi zake (TARI MLINGANO& ASA) wamesema ipo tayari kusaidia wakulima wa zao la ngano waweze kuzalisha kwa tija ili kukuza kilimo hicho wilayani hapa sambamba na uchumi wa mkulima.

@wizara_ya_kilimo kupitia ASA imetoa mbegu tani 80 kwa wakulima wa ngano mwezi Februari mwaka huu, huku @official_taritanzania wakiwa tayari wametoa mafunzo kwa maafisa ugani kwa lengo la kuongeza uelewa wa namna ya upimaji wa afya ya udongo.

Mkurugenzi wa TARI MLINGANO Tanga DKT. Catherine Senkoro akiwa na Mwandishi wa Kitulo FM kwenye shamba la Mfano la Ngano Kigala