Kitulo FM

Semina ya uwekezaji kwenye dhamana yafanyika kwa watumishi Makete

November 23, 2023, 9:29 am

Moja ya washiriki Mr Mbafu akiuliza maswali kwa wataalam kutoka BOT picha na Ombeni Mgongolwa

Ili kukuza uchumi kwa wananchi serikali kupitia BOT imetoa mafunzo kwa watumishi wa Umma juu ya Kuwekeza kwenye dhamana ya serikali ili kufaidi fulsa za uwekezaji serikalini.

Na Ombeni Mgongolwa

Luther Luvanda Mhasibu na mwezeshaji wa semina ya wadau juu ya uwekezaji kwenye dhamana za Serikali kutoka Bank kuu ya Tanzania Tawi la Mbeya amesema kuna faida kubwa ya kuwekeza kwenye dhamana ya Serikali kwa sababu inasaidia kukuza uchumi wa Nchi kwa kutoa fursa kwa wawekezaji mbalimbali ambao wataweza kuwekeza katika nchi.

Bi. Luvanda ameyasema hayo katika semina ya wadau juu ya uwekezaji kwenye dhamana za Serikali 2023/2024 iliyohusisha Watumsihi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo 22 Novemba, 2023 katika ukumbi wa H/w ya Makete

Luther Luvanda Mhasibu na mwezeshaji wa mafunzo kutoka BOT tawi la mbeya picha na Ombeni Mgongolwa

Aidha bi. Luvanda amesema kuwa dhamana hizi zinasaidia katika miradi mbalimbali ambayo inafanywa na Serikali, inayosaidia katika kujenga miundombinu bora na kuhakikisha mahitaji yote yanayotakiwa kwa wananchi kupatikana ili kujenga jamii ambayo ni bora.

Meneja mwezeshaji na Fedha wa BOT tawi la Mbeya Agathon Kipandula amesema lengo ni kutoa elimu kwa watumishi wote wa Serikali, Mashirika binafsi pamoja na wananchi wote huku akiwaasa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kuweka dhamana kwani kuna faida kubwa katika maisha na unajenga akiba ya kuitengeneza kesho yake kwa sababu inampa fursa ya kupata mkopo ambao utamwezesha kujikimu kwenye mahitaji yake muhimu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete Bi. Jack Jackline Mrosso ameishukuru Benki hiyo kwa kitoa elimu ya dhamana kwa Watumishi na kwamba imekuwa elimu itakayosaidia Watumishi kukabiliana na hali za kiuchumi wakati wowote

Kaimu Afisa Manunuzi Wilaya ya Makete Mathias Mbafu amesema mafunzo hayo yameonesha fursa kubwa kwa Watumishi kuwekeza fedha mahali salama zaidi kuliko mahali pengine na ameomba wameendee kutoa elimu hiyo mara kwa mara ili kusaidia kuongeza uelewa mpana juu ya dhana ya uwekezaji