Kitulo FM

Wafugaji Makete wapigwa marufuku kuingiza mifugo eneo la hospitali

September 11, 2023, 12:50 pm


Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya Makete Dkt. Kitundu akizungumzia kuhusu mazingira ya hospitali ya wilaya

Juhudi za kuendelea kutoa elimu kwa wananchi zinaendelea kutunza mazingira kwa kutopeleka mifugo katika eneo la hospitali.

Furahisha Nundu – Makete

Wakazi wa kata ya Iwawa wilaya ya Makete mkoani Njombe wametakiwa kutunza miundombinu na vifaa vya ujenzi katika Hosptitali ya Wilaya pamoja na kuacha kufunga mifugo yao kuzunguka eneo la hosptitali hiyo.

Wito huo umetolewa na Dkt. Kitundu kwa niaba ya Mganga Mkuu wa wilaya Makete akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye ofisi za kata ya Iwawa Makete mjini wakati wa kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi katika kata hiyo.
Dkt. Kitundu amesema wapo baadhi ya wananchi ambao wanafanya vitendo ambavyo vinarudisha nyuma jitihada za serikali katika kufanikisha miradi inayotekelezwa kwa kuiba vifaa vya ujenzi unaondelea katika hospitali pamoja na kufunga mifugo katika maeneo hayo jambo ambalo linaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu kama mifumo ya maji na umeme.

Mganga mfawidhi hospitali ya wilaya Makete Daktari Kitundu

Wakati huohuo Dkt. Kitundu ameishukuru serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya hospitali ya wilaya Makete.

Mganga mfawidhi hospitali ya Makete Dkt. Kitundu