Kitulo FM

Milioni 275 zimejenga Stendi ya Mabasi na Maegesho ya Malori Mfumbi.

January 24, 2023, 6:37 am

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe amesema ujenzi wa Stendi ya Mabasi naa maegesho ya Malori ipo mbioni kuanza kutumika baada ya kukamilika kwa kiasi kikubwa kwa huduma muhimu katika Stendi hiyo iliyopo kijiji cha Kimani Kata ya Mfumbi Wilayani Makete.

Ujenzi wa Stendi hii ulianza 2021 kwa kutumia fedha za mapato ya ndani ambapo mpaka kufikia sasa imegharimu zaidi ya shilingi Milioni 275 kwa lengo la kuongeza mapato ya Halmashauri.

Kamati ya Siasa CCM ngazi ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Ndg. Clement Ngajilo imepongeza jitihada za Uongozi Wilaya ya Makete kwa ubunifu wa mradi huo ambao baada ya kuanza kwake utakuwa ni chachu ya kukuza mapato ya Serikali.

Mpaka sasa Stendi hiyo imejengwa Kituo cha Polisi, Jengo la kukusanyia ushuru, Choo cha kulipia, Taa 17 zimefungwa na ukamilishaji wa Jengo la Abiria utakamilika siku 10 zijazo na kuruhusu Mabasi kuendelea kutoa huduma eneo hili.

Pia Makufwe ameongeza kuwa utaratibu wa wananchi kujenga vibanda kwa ajili ya Biashara utatangazwa siku chache zijazo naa kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kutumia fursa hiyo kukuza kipato chao.