Kitulo FM

Kamishna msaidizi, mkuu wa hifadhi ya Kitulo kuchangia mifuko 10 ya saruji Veta Makete

November 27, 2023, 7:24 pm

Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo kwenye mahafali ya chuo cha veta.picha na shafii

kutokana na jitihada za serikali kuendelea kujenga vyuo vya veta nchini imekuwa ni chachu kwa vijana kunufaika na mafunzo hayo katika kujiinua kiuchumi

na shafii

Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika maafali chuo cha Veta wilaya Makete Theodora Batiko amewaasa wahitimu kukitumia kile ambacho wamefundishwa na  kuwa wabunifu zaidi kwenye Yale yote walio fundishwa na walimu wao.

Amesema hayo kwenye mahafali ya 19 ya chuo cha veta wilaya ya makete yalio fanyika chuoni hapo ambapo amewataka wazazi na walezi kuendelea  kuwasomesha watoto kwa lengo la kulea familia zao

Aidha bi. Theodora amesema lazima watoto wafundishwe wakiwa bado wadogo huku wazazi wakitakiwa kuwapa nafasi watoto wao kwenye kila wanacho taka kusomea huku akiahidi kutoa mifuko kumi ya saruji kwaajili ya kujenga bwalo la chakula ambalo imekua changamoto katika chuo hicho.

Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo bi. Theodora

Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo pamoja na baadhi ya viongozi katika mahafali katika chuo cha veta makete

Mkuu wa chuo cha veta wilaya makete ndg. Elisha Nkuba amesema wahitimu wameandaliwa vyema na hanashaka  kwani wana vigezo vyote kuingia kwenye soko la ajira

Aidha mkuu huyo wa chuo amemuomba mgeni rasmi ufadhili wa wanafunzi wakike ambao watajifunza katika chuo hicho kwa kuwa kina miundombinu  ambayo inamwezesha mwanafunzi wa kike kusoma.

sauti ya mkuu wa chuo veta ndg Elisha

viongozi mbali mbali wakiongozwa na Kamishna msaidizi na mkuu wa hifadhi ya kitulo katika ukaguzi wa namna mafunzo kwa vitendo yanafanyika katika moja ya darasa chuoni hapo

Nae mkuu wa polisi jamii wilaya makete inspekta Hassan Lujendo amewaasa wanafunzi wano hitimu kuwa makini kwenye Yale walio fundishwa na kuyatumia vizuri

Hata hivyo inspekta Hassan amewaasa madereva piki piki maarufu boda boda kupata mafunzo ya udereva na kupata leseni pamoja na kukata Bima kwaajili ya pikipiki ili kujilinda na matatizo yatakayo tokea kama ajali au kuunguliwa na chombo cha moto.

mkuu wa polisi jamii wilaya makete inspekta Hassan