Kitulo FM

waliokata rufaa Tasafu kuhakikiwa upya

September 21, 2023, 10:29 am

maafisa wa Tasaf wilaya ya Makete wakitoa taarifa ya zoezi lauhakiki wa wanufaika wa mpango wa Tasaf picha kushoto ni mratibu wa tasafu Wilaya John Subeth na kulia ni Herry Mpunza Afisa ufuatiliaji wa miradi ya TASAF (W) Makete.na Furahisha Nundu

kupitia rufaa ya wanufaika wa mpango wa Tasaf wilaya ya Makete,timu ya wataalamu kutoka Halmashauri ya wilaya ya Makete wameanza zoezi la kuhakiki taarifa katika baadhi ya kata za wilaya ya Makete.

na Aldo Sanga

TASAF Wilaya ya Makete imeanza zoezi la uhakiki kwa walengwa wa TASAF waliokata Rufaa ili kuwa wanufaika katika Kata mbalimbali za Wilaya ya Makete na zoezi hilo limeanza leo tarehe 21 Septemba na litakamilika tarehe 23 Septemba 2023.

Akizungumza na Kitulo FM Herry Mpunza Afisa ufuatiliaji wa miradi ya TASAF (W) Makete amesema zoezi hili ni muhimu katika kuhakikisha Serikali inawafikia walengwa wote ili kupambana na hali za Uchumi wa Wananchi hao katika maeneo yao na kuwasihi watoe taarifa sahihi ili kufikia lengo la Serikali.

Herry Mpunza Afisa ufuatiliaji wa miradi ya TASAF (W) Makete

John Subeth Mratibu wa TASAF (W) amesema TASAF imenufaisha walengwa wengi katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Makete na wanatarajia miaka kadhaa ijayo kuanza kuwahitimisha walengwa ambao wameonesha kupata mafanikio zaidi katika kupambana na hali ya Umasikini.

maafisa wa Tasaf wilaya ya Makete wakitoa taarifa ya zoezi lauhakiki wa wanufaika wa mpango wa Tasaf picha kushoto ni mratibu wa tasafu Wilaya John Subeth na kulia ni Herry Mpunza Afisa ufuatiliaji wa miradi ya TASAF (W) Makete.na Furahisha Nundu

Pia Subeth amesema TASAF (W) ya Makete imeanza kutoa Elimu kwa walengwa ya namna ya kuandaa mpango biashara ili baada ya kuhitimu walengwa waweze kunufaika na mpango huo na kuwasaidia katika Biashara ambapo mpango huo umeanza katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kijiji cha Ivilikinge Kata ya Isapulano

John Subeth Mratibu wa TASAF Wilaya ya Makete

Wilaya ya Makete inajumla ya walengwa 4,553 wanaonufaika na TASAF ambapo wamepungua kutoka zaidi ya 4,628 kwa sababu mbalimbali ikiwemo vifo na wengine kuhama