Kitulo FM

DC Sweda ampa kongole Rais Samia kwa miradi Makete

January 19, 2024, 5:56 pm

dc sweda akiwa katika jiko la shule matamba sekondari picha na mwandishi wetu

na mwandishi wetu

kutokana na fedha nyngi kutolewa na serikali viongozi mbali mbali na wananchi wahimizwa kutunza miradi hiyo

Mkuu  wa wilaya ya  makete mh Juma Sweda amemshukuru Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mh Samia Suluh Hassani kwa kutoa fedha kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika maeneo mbali mbali huku akiwataka viongozi wa maeneo husika kuwajibika katika kuyatunza

Mh sweda ameyasema hayo alipokuwa matamba sekondari   kukagua mabweni katika shule hiyo, huku akimpongeza mkuu wa shule matamba kwa ubunifu alioufanya katika kuhakikisha jiko la shule hiyo linajengwa katika ubora pamoja na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano katika kufanikisha ujenzi wa jiko hilo unakamilika

sauti ya dc sweda

kutokana na malalamiko ya wananchi kuhusu wazazi kuwanunulia pikipiki watoto imekuwa ikichangia watoto hao kutofika shule mh sweda ametaka kukamatwa kwa pikipiki zote zilizonunuliwa kwaajili ya watoto hao ili waweze kurudi shule

dc sweda vs wananchi

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Matamba mh Nyambu ameishukuru Serikali inayoongozwa na mh Samia Suluhu Hasani kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuhakikisha miradi mbali mbali inatekelezwa katika kata ya matamba

Sauti ya diwani matamba

Nao baadhi ya wananchi pamoja  viongozi wa chama ngazi ya kata wamemshukuru mkuu wa wilaya kwa kazi kubwa anayoifanya yakuhakikisha wananchi wake wanapata maendeleo

sauti za wananchi na viongozi wa chama

katika ziara hiyo mh mkuu wa wilaya ameridhishwa na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja  katika shule ya msingi iwale,madarasa mawili ya awali katika shule ya msingi kinyika huku akionyesha kutokuridhishwa na milango iliyopo katika madarasa shule ya sekondari matamba na mkutaka mkuu wa shule kuhakikisha  anakwenda kujifunza kwa mkuu wa shule ya  msingi iwale