Kitulo FM

Watendaji wa kata na vijiji hamasisheni upatikanaji wa Mbogamboga na matunda shuleni

19 June 2026, 6:01 pm

Afisa Tarafa wa Tarafa ya Ikuwo, Ndg. Albert Luwondo

wazazi wametakiwa kuwa mstari mbele kuchangia chakula shuleni ili kufanikisha watoto wanapata chakula mara mbili tofauti na hivi sasa ambapo wanafunzi wanapata mlo mmoja pekee

na mwandishi wetu

Watendaji wa Kata pamoja na Vijiji wametakiwa kuhakikisha kuwa wanahamasisha wazazi ili wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wanapata chakula mara mbili kwa siku, sambamba na kuboresha upatikanaji wa Mbogamboga na matunda katika taasisi hizo za Elimu.

Hayo yamebainishwa na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Ikuwo, Ndg. Albert Luwondo,a akiwamwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Makete,  Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa, kwenye kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe, kilichofanyika katika Ukumbi wa Bomani.

afisa lishe wilaya ya makete bi.Jackiline nanauka akitoa maelekezo kwenye kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe

Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete,  Ndg. Jerry Daimon Mwaga, amwasihi watendaji hao kuhakikisha kuwa wazazi na walezi wahamasishwe kuzitumia mashine zilizopo jirani na vijiji vyao ili kupata Unga wenye Virutubisho kwaajili ya matumizi ya watoto mashuleni na nyumbani.

Ikumbukwe kuwa kikao hicho cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa ngazi ya Wilaya, kimelengea kujadili na kupokea taarifa za Utekelezaji wa Afua za Lishe kwa ngazi za Kata, pamoja kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa Udumavu unakomeshwa ndani ya Wilaya.