Kitulo FM
Kitulo FM
22 July 2026, 9:33 am

Kutokana na umuhimu mkubwa wa umeme katika makazi ya watu na hata katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali wakazi wa kijiji cha Usagatikwa wameonyesha kutoridhishwa na baadhi ya watu kuharibu miundombinu ya umeme na kupelekea kukosa umeme kwa mda wa wiki mbili huku wakienda mbali wakitaka uwajibishaji kwa hao wanaoharibu miundombinu.
Na Mwandishi Wetu.
Wananchi wa kijiji cha Usagatikwa wilayani Makete mkoani Njombe wameomba hatua kali zichukuliwe kwa wananchi wenzao ambao wamekuwa wakiharibu miundombinu ya umeme na kupelekea umeme kukosekana kijijini hapo.
Wananchi hao wamesema hayo kwenye mkutano wao na Diwani na kudai ukosekanaji wa umeme unaosababishwa na baadhi kuharibu miundombinu ya umeme unapelekea adha kubwa kwao.

Akijibu kero hiyo Diwani wa Kata ya Tandala Egnatio Mtawa amesema wananchi wanapaswa kulinda miundombinu ya umeme hasa wakati wa kukata miti, na kama kuna ulazima kwa kukata miti iliyopo jirani na miundombinu ya umeme, watoe taarifa kabla kwa uongozi wa kijiji ili zifikishwe TANESCO ambapo watakuja kushirikiana na mhusika bila kuharibu miundombinu hiyo.
Amesema ni muhimu wananchi wakatunza miundombinu kwa kuwa inapoharibika wao ndio watapata madhara makubwa.