Kitulo FM
Kitulo FM
24 June 2026, 9:30 am

katibu tawala mkoa wanjombe Dkt Stephen Nindi
umoja ni nguvu utengano ni udhaifu ni kauli iliyojidhihilisha kwenye baraza maalumu la madiwani la kupokea na kujadili hoja za mdhibiti na maguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) jambo lililopelekea halmashauri kupata hati safi
na mwandishi wetu
Halmashauri ya wilaya ya makete mkoani njombe imetakiwa kutoa vielelezo kamili ili kufuta baadhi ya hoja zilizojitokeza kwenye ripoti ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG).
haya yamesemwa hii leo na katibu tawala mkoa wanjombe Dkt Stephen Nindi alipo muwakilisha mkuu wa mkoa wa Njombe mh. Antoni Mtaka kwenye baraza maalumu la madiwani la kupokea na kujadili hoja za mdhibiti na maguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ambapo katibu tawala mkoa wa njombe amebainisha baadhi ya hoja ikiwemo kuongeza juhudi zaidi kwenye urejeshaji wa madeni ya vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.
sauti ya nindi 01
Hata hivyo ametoa maelekezo kwamba nilazima halmashauri iendelee kutenga asilimia 40 ya mapato ya ndani kwenye shunguli za maendeleo na kulipa madeni kwa wakati ya baadhi ya watumisha na wazabuni mbalimbali .
sauti ya nindi 02

mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya makete Rabison Mahenge
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mfamasia Rabson Mahenge, amesema kuendelea kupata hati safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kunawapa nguvu ya kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudumisha ushirikiano uliopo.
Mhe. Mahenge amesema mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi za pamoja zinazofanywa na viongozi, madiwani, wataalamu, watendaji pamoja na wananchi wa Makete katika kusimamia majukumu ya halmashauri.
sauti ya halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mfamasia Rabson Mahenge

baadhi ya madiwani wakiwa katika baraza maalumu la madiwani la kupokea na kujadili hoja za (CAG)
Amesema Hati Safi ni ishara ya uwajibikaji na usimamizi mzuri wa rasilimali za umma, hivyo viongozi wataendelea kushirikiana ili kuhakikisha mafanikio hayo yanaendelea kupatikana.
Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano huo utaendelea kuwa chachu ya kuitangaza Makete kwa sifa nzuri za kiutendaji na kuleta maendeleo yenye manufaa kwa wananchi.
baadhi ya waheshimiwa madiwani wamemshukuru katibu tawala wa mkoa wa njombe kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa njombe kwa namna ambavyo amewashauri namna bora ya kufuta hoja hizo kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesbau za serikali
sauti ya Diwani