Kitulo FM

Madalali wa mazao makete waaswa kufuata utaratibu katika kutekeleza majukumu yao

19 June 2026, 6:35 pm

viongozi pamoja na madalali wakiwa kwenye kikao cha madalali

kutokana na wakulima wengi kulalamika kuhusu madalali wa mazao, halamshaur ya makete imeanzisha umoja wa madalali wa mazao makete ambao watambulika rasmi katika ufanyaji kazi wa udalali ili kuepusha malalamiko ya wakulima kuhusu madalali

na mwandishi wetu

Umoja wa madalali wa mazao wilayani makete mkoani njombe wametakiwa kufanya kazi zao kwa kushirikiana na uongozi uliochaguliwa ili kubaini madalali wanaofanya kazi hizo bila kusajiliwa

Hayo yamesemwa hii leo juni 19,2026 na afisa kilimo,mifugo na uvuvi wilaya ya makete ndg Evance mdee baada ya kukutana na umoja wa madalali hao kwenye ukumbi wa mamlaka ya mji mdogo wa iwawa kwa lengo la kujadili mambo mbali mbali  ikiwa ni pamoja na kuwachagua viongozi wa umoja huo kwa ngazi ya wilaya na tarafa

mwenyekiti wa umoja wa madalali wilayani makete

Amesema kuwa madalali ambao watafanya kazi bila kufuata utaratibu sheria zitachukuliwa kwani wamekuwa wakiwadhurumu wakulima na kupotosha soko la mazao  na kuutaka uongozi huo uliochaguliwa kuhakikisha madalali wote wa mazao wanafanya kazi zao kwa kufuata utaratibu uliowekwa

sauti ya afisa kilimo evance mdee

madalali wa mazao mbali mbali wilayani makete wakiwa kwenye kikao cha madalali

Akizungumza kwa niaba ya viongozi waliochaguliwa kwenye kiako hicho mwenyekiti wa madalali wa mazao wilaya ya makete ndg Denmark Mahenge pamoja na mhasibu  Betrice Kyando wameahidi kushirikiana na madalali wote ili kurahisisha utendaji wao wa kazi huku wakisisitiza yaliyojadiliwa yatafanyiwa kazi  ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua madalali watakaofanyakazi kinyume na utaratibu uliowekwa

sauti ya mwenyekit vs mhasibu

miongoni mwa dalali akichangia hoja kwenye kikao

Kwaupande wake mratibu wa madalali wa mazao wilaya ya makete ndg Mathayo Msokwa amesema kuwa umoja huo wa madalali utakuwa chachu kubwa ya kuwasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa bei inayotakia huku akiwataka kushirikiana ili kuthibiti madalali ambao hawajasajiliwa kufanya kazi hiyo

Ikumbukwe kuwa mwenyekiti wa madalali wa mazao wilaya ya makete Denmark Mahenge alipata kura 30, huku katibu ni Zephania Mtaita akipata kura 29 na muhasibu Betrece Kyando akipata kura 41