Kitulo FM

Wananchi wa ikonda walia na changamoto ya barabara

22 July 2026, 10:13 am

Wananchi wa kijiji cha Ikonda

kutokana na umuhimu mkubwa wa miundombinu ya barabara katika maeneo mengi hapa nchini, wakazi wa kijiji cha ikonda wamewasilisha changamoto ya barabara ambazo zimekuwa zikiwaletea adha kubwa katika shughuli zao za kila siku hasa wakati wa masika na kuimba serikali iweze kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.

na mwandishi wetu.

Wananchi wa kijiji cha Ikonda wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujiandaa kushirikiana kwa pamoja kufanya matengenezo ya daraja maarufu la kwa Swallo ili kurahisisha upitikaji wake hasa kwa watoto wanaosoma katika shule ya msingi Ikonda

Katika mkutano wa Diwani na wananchi wa kijiji hicho Christina Mahenge, Osward Sanga na Tegemea Sanga wamemueleza uwepo wa changamoto za kupitika madaraja ya barabara za mitaa katika kijiji hicho pamoja na nyingine kutopitika hasa kipindi cha masika

wananchi kijiji cha ikonda

Akizungumza wakati akijibu kero hizo za wananchi, Diwani wa kata ya Tandala Egnatio Mtawa amesema sio kila jambo la maendeleo linatakiwa kusubiri serikali ifanye, hivyo wanatakiwa kufanya na serikali itakuja kuwaunga mkono wakiwa wanatekeleza

Kuhusu barabara ya kupita kwa Swallo diwani amesema si wakati wa kusubiri matatizo yatokee ndipo hatua zichukuliwe hivyo wananchi wanatakiwa kujiandaa kushirikiana naye kufanya maendeleo katika barabara hiyo pale itakapotangazwa

diwani mtawa barabara

Diwani Mtawa anaendelea na mikutano katika vijiji vya kata yake kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika maeneo yao.