Kitulo FM

CCM Makete yafanya uchaguzi wa vijana chipukizi

September 25, 2023, 8:41 am

vijana wa chipukizi wakiwa na kadi za uanachama na viongozi wa jumuiya ya vijana CCM wilaya.na mwandishi wetu

katika kuwaandaa vijana wazalendo na viongozi wa baadaye chama cha Mapinduzi CCM Makete kimefanya uchaguzi wa viongozi wa vijana hao huku nafasi ya mweneyekiti ikichukuliwa na Michael Kened Chaula .

na :Rose Njilile

Jumuiya ya Vijana Makete mkoani Njombe kupitia Chama cha Mapinduzi Ccm imefanya Chaguzi wa chipukizi katika Ofisi ya Chama hicho

Uchaguzi huo ambao ulihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa vijana Wilaya ya Makete ulikuwa na jumla ya wajumbe wapatao 50 ambao ulikuwa na lengo la kumpata Mwenyekiti wa Chipukizi,wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji, pamoja na Wajumbe wa mkutano Mkuu

Tamson mbilinyi ni Mwenyekiti wa Vijana Makete amesema kuwa Uchaguzi huo ni kuwaandaa vijana chipukizi kuanzia umri mdogo  ili waweze kujiimarisha kwenye misingi ya chama hicho

sauti ya Tamson mbilinyi mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Makete

AIDHA mwenyekiti huyo wa vijana  amesema kuwa imekuwa ni utaratibu wa jumuiya ya vijana wa kuwaandaa viongozi bora  wa baadae ambao watalisimamia na kuongoza Taifa la Tanzania kwa ujumla

sauti ya Tamson mbilinyi mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Makete

Ndg Hassan kapolo ni Katibu wa vijana makete na hapa  anatangaza matokeo ya wagombea wa ngazi mbali mbali  za chipukizi mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo

sauti ya katibu wa Jumuiya ya vijana Ndg Hassan kapolo
viogozi wa Chipukizi baada ya uchaguzi kukamilika. na mwandishi wetu

Nao baadhi ya viongozi waliochaguliwa akiwemo Michael Kened Chaula pamoja Gospo Imannuel Chande wamewashakuru wajumbe kwa kuwachagua na kuahidi kutekeleza yote yanayokusudiwa kufanyika kwa manufaa ya chipukizi wilaya ya makete na mkoa kwa ujumla

sauti ya viongozi wa Chipukizi baada ya kuchaguliwa katika nyasifa hizo