Kitulo FM

Miundombinu shule ya sekondari ya wasichana Makete sasa shwari

October 2, 2023, 8:32 am

Mwonekano wa madarasa ambayo yamekamilika kujengwa .Picha na Furahisha Nundu

Kupitia ongezeko la wanafunzi hususani kidato cha tano na cha sita serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 1 kujenga madarasa shule ya sekondari ya wasichana Makete.

na Furahisha Nundu

Kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni 50 zimetolewa na serikali kwa ajili ya kujenga madarasa, bweni na vyoo shule ya sekondari ya wasichana Makete.

Fedha hizo zimetolewa kupitia miradi ya EP4R kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu katika shule hiyo ikiwa ni miundombinu kwa ajili ya kidato cha tano na cha sita ikiwemo madarasa 10, vyoo matundu 10 na mabweni matano.

Baadhi ya viongozi wa serikali akiwemo mkurugezi mtendaji (W) Makete Bw,William Makufwe mbele na mbunge wa jimbo la Makete Mh. Festo Sanga nyuma yake. Picha na Furahisha Nundu

Kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo Mwl. Sayuni Sanga amesema ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa umekamilika huku akiongeza kuwa ujenzi wa vyoo na bweni upo katika hatua za mwisho.

Shule la sekondari ya wasichana Makete ina jumla ya wanafunzi 607 kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.