Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Makete wafanya Kikao maalumu kujadili taarifa ya fedha mwaka 2022/2023
Kitulo FM

Madiwani Makete wafanya Kikao Maalumu kujadili taarifa ya Fedha 2022/2023

August 31, 2023, 2:11 pm

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Makete leo August 31, 2023, limepitisha taarifa ya ufungaji wa Hesabu kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Akizungumza kwenye Kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mhe. Christopher Fungo hicho kilichojadili uwasilishaji wa taarifa ya Ufungaji wa Hesabu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 amesema Baraza kwa umoja wake limepitisha taarifa hiyo.

“Baraza limeridhia taarifa hii pamoja na ushauri ambao Waheshimiwa Madiwani wameutoa tutaendelea kuufanyia kazi kwa ajili ya maboresho zaidi katika utendaji kazi”

Kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete kimehudhuriwa na Ndg. Ben Sahehe Mkaguzi kutoka Ofisi ya CAG, Bi. Anastanzia Kibona Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Usimamizi na ukaguzi Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Njombe, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji H/W Makete Ndg. Humphrey Mushi, Waheshimiwa Madiwani, pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.

Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Makete wafanya Kikao maalumu kujadili taarifa ya fedha mwaka 2022/2023