Mbunge Sanga aunga jitihada za wadau kwenye Elimu
Kitulo FM

Mhe. Sanga aungana na wadau kukarabati Shule Unenamwa-Makete

July 4, 2023, 8:20 am

Mbunge Jimbo la Makete Mhe. Festo Sanga amekabidhi shilingi Laki 5 na elfu 70 kwa Uongozi wa Shule ya Msingi Unenamwa kukarabati Madarasa ya shule hiyo

Mhe. Sanga amekabidhi fedha hizo ambazo zitasaidia kwenye ukarabati wa Madarasa ambayo Wadau wa Kijiji cha Unenamwa na Usililo Kata ya Luwumbu wameanza kufanya ukarabati wa Madarasa hayo ambayo yamechakaa

Wananchi wa Kijiji cha Unenamwa wamemshukuru Mhe. Mbunge kwa kisaidia ukarabati wa Madarasa hayo na kuunga mkono jitihada za Wadau wa Maendeleo Kata ya Luwumbu.

Mhe. Sanga ameendelea na Ziara ya Kijiji kwa Kijiji katika Kata ya Luwumbu inayojumuisha Kijiji cha Uganga, Luwumbu, Lugawo, Unenamwa na Usililo

Wakati huohuo amekabidhi shilingi Laki 3 na nusu Kwa Uongozi wa Kijiji cha Uganga kwa ajili ya kununua Betri la Sola kwenye Zahanati ya Kijiji hicho baada ya kufika na kusikia changamoto ya Wagonjwa kuhudumiwa usiku bila mwanga wa Taa.