DED Makete akikagua Lumbesa ya Viazi Geti la Mfumbi
Kitulo FM

Ukaguzi wa Mapato Geti la Mfumbi Makete

March 3, 2023, 2:51 pm

Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Wilaya Makete William Makufwe akikagua Magari ya Mizigo namna madereva na wamiliki wanavyolipa Mapato ya Halmashauri kwenye Geti la Mfumbi ambapo Magari mengi yanayobeba Viazi kutoka Ikuwo na Matamba hupita njia ya Mfumbi.

Akiwa getini hapo Makufwe ameangalia pia hali ya Lumbesa na kuwasihi wakulima na wanunuzi kununua vifungashio vinavyoweza kubeba Viazi kwa Kilo 100 ili kuondoa Malalamiko ya wakulima kuwa wanaibiwa kupitia Lumbesa kwani vifungashio vinavyotumika hivi sasa pamoja na kujaza Viazi na kulazimisha kushonea juu lakini havifiki uzito wa Kilo 100.

Pia amewataka Wafanyabiashara kuwa waaminifu kwa kulipa Ushuru ili kuongeza Mapato ya Serikali ambayo yatasaidia kutekeleza miradi na shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe akiangalia Magunia ya Viazi geti la Mfumbi
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete William Makufwe akiangalia Magunia ya Viazi geti la Mfumbi