Kitulo FM

Wananchi Makete waishukuru serikali kutoa pembejeo kwa wakati

September 19, 2023, 9:21 pm

Baadhi ya wakulima wakiwa kwenye moja ya kituo cha kutolea huduma za pembejeo Iwawa Makete mjini.na Aldo Sanga

Kuelekea msimu wa kupanda mazao wananchi wameendelea kujitokeza katika vituo vya pembejeo kwa ajili ya kuchukua mbolea, ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutangaza wakulima kuhakiki taarifa zao.

Na Aldo Sanga.

Wananchi wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo vya pembejeo za kilimo ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutoa wito wa kuhakiki taarifa zao kwenye daftari la wakulima Makete. Wakizungumza juu ya zoezi linaloendelea nchini kote baadhi ya wakulima wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo.

Sauti za baadhi ya wakulima waliojitokeza kwenye vituo vya pembejeo Iwawa Makete mjini

Kwa upande wake Jonasko Sanga ambaye ni miongoni mwa wasambazaji wa pembejeo amekiri kuwepo kwa mwitikio mkubwa wa wakulima huku akiwataka wakulima kuchukua pembejeo kulingana na taarifa zao za usajili.

Wakala wa pembejeo Bw. Jonasko Sanga akiwa kwenye kituo cha kutolea pembejeo akihudumia wakulima.na Aldo Sanga

Bw. Jonasko Sanga ameongeza kuwa kwa wale ambao taarifa zao za awali zilikua na idadi ndogo ya mahitaji kwenda katika ofisi za serkali ya kijiji kuongeza mahitaji yao.

Sauti ya Jonasko Sanga wakala wa pembejeo Iwawa Makete mjini