Mwenyekiti wa NPC Damiani Kunambi aliyesimama akizungumza na wananchama wa NPC
Kitulo FM

Waandishi wa Habari wakutana Mkoani Njombe

December 30, 2022, 6:54 am

 

Mwenyekiti wa NPC Damiani Kunambi aliyesimama akizungumza na wananchama wa NPC

Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Njombe, Njombe press club NPC kimefanya mkutano mkuu mkoa humo huku agenda kuu za mkutano huo mkuu ikiwa ni Marekebisho ya katiba pamoja na kubariki uongozi wa muda ulio kuwa umechaguliwa kuendelea baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wake.

Hatua hiyo imefikiwa mwishoni mwa mwezi huu Disemba, 2022  ambapo mkutano huo kwa umoja wa wananchama wake umetoa baraka kwa viongozi wa muda ambao walichaguliwa kutokana na changamoto zilizo kuwepo katika chama hicho kufanya kazi zilizo waridhisha wanachama.

Aidha mkutano huo kwa kujali na kuzingatia masilahi ya chama mkoani Njombe (NPC) umefanya marekebisho ya KATIBA yake illi kuongeza umakini na uhai wa chama na wanachama wake

Katika hatua nyingine mkutano huo kwa kauli moja umeweka vipaumbele vya kuimarisha vyanzo vya mapato vipya vitakavyo imarisha uchumi wa Chama hicho wakati wote