Afisa Maendeleo ya Jamii (W) ya Makete Bi. Jackline Mrosso
Kitulo FM

Elimu ya mikopo imetolewa kata zote wilaya Makete-Afisa maendeleo wilaya

June 21, 2023, 8:08 am

Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Makete Bi. Jacklin Mrosso amesema halmashauri inaendelea kutoa elimu ya mikopo kwa jamii lengo likiwa ni kuhakikisha jamii inaelewa fursa zilizopo na kuzitumia.

Akizungumza na Kitulo FM, Mrosso amesema idara hiyo imetoa elimu kuhusu mikopo ya 10% na mikopo ya wizara katika kata zote 23 za wilaya ya Makete ambapo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu wamekopeshwa fedha nyingi tofauti na miaka iliyopita

Mrosso amesema halmashauri imepiga hatua kubwa ya kukopesha mikopo mikubwa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuachana na mikopo midogo isiyo na tija.

Vilevile amewataka waliokopeshwa kuhakikisha wanarejesha fedha hizo kwa uaminifu mpaka kufika tarehe 15 Julai, 2023 wawe wamekamilisha ili kutoa fursa ya kukopesha vikundi vingine vinavyohitaji kupata mkopo.