Aliyesingiziwa kufariki na kufufuka, afariki leo
Kitulo FM

Aliyedhaniwa kufariki juzi na kufufuka, afariki leo

June 13, 2023, 8:10 am

Bi. Felister Sanga aliyedhaniwa kufariki juzi na kufufuka kijiji cha Ipepo kata ya Ipepo wilayani Makete amefariki alfajiri ya leo Juni 13, 2023.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Dkt. Jonathan Kitundu kwa niaba ya mganga mkuu wilaya ya Makete ambapo amesema wataalam hutoa taarifa za kuthibitisha kifo cha mtu baada ya saa moja kupita tangu mapigo ya moyo yanapoacha kufanya kazi kabisa na si mtu yeyote anaruhusiwa kutangaza bila kuthibitishwa taarifa za kifo cha mtu na wataalam kama ilivyofanyika na ndugu zake siku moja iliyopita na kuzua taharuki

Ikumbukwe marehemu alikuwa anasumbuliwa na afya yake kwa muda mrefu na alipopelekwa hospitali ya Ikonda mwishoni mwa wiki jana na kulazimika kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi, ndugu walikataa kwa madai kwamba hawana uwezo wa kumhudumia kifedha na kuamua kurudi naye nyumbani ambapo alfajiri ya leo amepoteza uhai.