Sungusungu Tusilete usumbufu kwa Wananchi- Insp. Lujendo
Kitulo FM

Sungusungu msiwasumbue raia-Insp. Lujendo

June 13, 2023, 8:48 am

Akizungumza na Kitulo FM, Mkuu wa Polisi Jamii wilaya ya Makete Inspekta Hassan Lujendo amesema ulinzi shirikishi ni muhimu sana katika jamii kwa lengo la kuongeza amani kwa wananchi.

Inspekta Lujendo amesema jeshi la polisi linahitaji kufanikisha hali ya amani na ulinzi kwa wananchi wake hivyo ulinzi shirikishi ni muhimu kwa jamii katika kuongeza ufanisi wa ulinzi na usalama kwa raia.

Vilevile amelitaka jeshi la ulinzi shirikishi wilayani hapa (Sungusungu) kufanya kazi kwa misingi ya maadili, uzalendo na upendo na kutoleta usumbufu kwa wananchi kwani wao wanapaswa kuhakikisha jamii inakuwa salama wakati wote.