Kitulo FM

DC Sweda aahidi laki tano matengenezo barabara Kinyika-Mlondwe

January 19, 2024, 6:30 pm

DC Sweda akiwa na viongozi wa kata katika kukagua barabara hiyo ya Nyika- Mlondwe. Picha na mwandishi wetu

na mwandishi wetu.

Imeelezwa kuwa barabara ni moja ya njia inayowasaidia wanananchi kuweza kujikwamua kiuchumi.

mkuu wa wilaya makete mh juma sweda ametembela barabara  ya kinyika- mlondwe na kuona changamoto inayowakumba wanachi wa maeneo hayo  na kuahidi  kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwaajili ya mfuta ya gari litakalotumika kutengeneza eneo hilo korofi pamoja na kuwataka kuweka makaravati katika eneo hilo

hayo yamejiri baada ya wananchi wananchi wa kata ya kinyika wamemuomba mkuu wa wilaya makete mh juma sweda  aweze kuwasidia  kuondokana na adha wanayoipata ya  changamoto ya barabara ya kinyika – mlondwe katika kitongoji cha idofi ambapo mkuu wa wilaya amesema kuwa hatua za utengenezaji ziwenze kuanza kwa kuhakikisha makaravati yanawekwa katika maeneo hayo

moja ya mwananchi akiwa katika barabara hiyo

wananchi hao mbele ya mkuu wa wilaya katika mkutano uliofanyika katika shule ya sekondari kinyika kwamba barabara hiyo imekuwa ikiwaleatea changamoto kubwa kutokana na mvua zinazoendela kunyesha na kushindwa kusafirisha mazao yao kwa wakati

sauti za wananchi

kwa upande wake kaimu meneja wa tarura ndg kawogo amekiri kuwapo na changamoto hiyo huku akiwata kuwa na subira pindi ambapo jitohada zinazoendela kufanyika ili kufanikisha adha hiyo inamalizika

sauti ya meneja wa tarura