Kitulo FM

Wananchi watakiwa kutunza miundombinu, vifaa vya ujenzi hosptitali ya wilaya Makete

September 15, 2023, 10:50 am

Daktari Kitundu kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya Makete akiwa kwenye

Wakazi wa kata ya Iwawa wilaya ya Makete mkoani Njombe wametakiwa kutunza miundombinu na vifaa vya ujenzi katika Hosptitali ya Wilaya pamoja na kuacha kufunga mifugo yao kuzunguka eneo la Hosptitali hiyo.
Wito huo umetolewa na Dkt. Kitundu kwa niaba ya Mganga Mkuu wa eilaya Makete akiwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye ofisi za kata ya Iwawa Makete Mjini wakati wa kutoa taarifa za utekelezaji wa miradi katika kata hiyo.
Dkt. Kitundu amesema wapo baadhi ya wananchi ambao wanafanya vitendo ambavyo vinarudisha nyuma jitihada za Serikali katika kufanikisha miradi inayotekelezwa kwa kuiba vifaa vya ujenzi unaondelea katika Hospitali pamoja na kufunga mifugo katika maeneo hayo jambo ambalo linaweza kusababisha uharibifu wa miundombinu kama mifumo ya maji na Umeme

sauti ya dr kitundu

WAKATI huo huo Dkt. Kitundu ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya Hospitali ya Wilaya Makete