Kitulo FM

DC Samweli Sweda ahimiza upandaji miti katika taasisi Mbalimbali Makete

January 24, 2024, 9:53 pm

mwonekano wa jengo la madarasa yaliyoezuliwa na upepo picha na mwandishi wetu

Kutokana na maafa yaliyotokea katika baadhi ya taasisi ikiwemo shule za Sekondari Mang’oto na Ipelele Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Samweli Sweda amewataka wananchi Kupanda Miti katika maeneo yote yenye Taasisi

Na Aldo Sanga

Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma Sweda,mapema hii leo Januari 23, 2024 amefika katika shule ya Sekondari Ipelele, iliyopo wilayani Makete, mkoani Njombe, baada ya kuezuliwa hapo jana jioni Januari 22, 2024, kulikosababishwa na mvua kali iliyoambatana na Upepo.
Akiwa katika aneo la tukio,Mhe, Sweda, amewataka wakazi wa maeneo hayo kuwa tabia ya kupanda miti, ambayo itakuwa msaada mkuwa katika kuzuia majanga ya kama hayo kutokea, ambapo kwa sasa wilayani Makete, imeonekana kukumbwa na janga hilo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete, Ndg. Clemence Mwamwite Ngajilo, amewataka wakazi wa maeneo hayo, kuchukua tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa na Upepo mkali, na kwamba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ipo pamoja nao katika kuhakikisha shule hiyo inarudi katika ubora wake wa hapo awali.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Mhe. Christopher Fungo, amewataka wananchi hao kuungana kwa pamoja kuhakikisha kuwa shule hiyo inajengwa na kurudi katika ubora wake wa hapo awali.

Hata hivyo, wakazi wa kata ya Ipelele, kwa pamoja wameunga mkono shughuli za ujenzi wa shule hiyo, kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni moja na elfu tatu, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Makete, Mhe. Juma Sweda na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Festo Sanga, wameahidi kutoa shilingi laki tano, na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bi. Jackline Mrosso,ameahidi kutoa shilingi laki tatu, ili kufanikisha ukarabati wa shule hiyo ya Sekondari Ipelele.

mbunge wa jimbo la makete Mh Festo Sanga alipotembelea eneo la maafa