Kitulo FM

Bodaboda Ndulamo wakabidhiwa viaksi mwanga

December 7, 2023, 12:49 pm

vijana wa bodaboda katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa viakisi mwanga.picha na shafii

Katika kukabiliana na ajali za barabarani vijana bodaboda wametahadharishwa kuwa makini wanapokuwa barabarani wakati wa usiku wakijitafutia kipato kutokana na matukio mbalimbali yanayotokea ya kiuharifu

na shafii

Madereva pikipiki (bodaboda) Wilayani Makete Mkoani Njombe wameshauriwa kufuata sheria za barabarani kwa dhumuni la kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.

Katika kukabiliana na ajali za barabarani wametahadharishwa kuwa makini wanapokuwa barabarani wakati wa usiku wakijitafutia kipato kutokana na matukio mbalimbali yanayo tokea ikiwemo wizi.

Jeshi la polisi wakiwa na vijana wa bodaboda baada ya kutoa elimu ya usalama barabani

Akizingumza wakati wa kukabidhi viakisi mwanga (reflector) kwa kikundi cha wasafirishaji wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda katika Ofisi ya kijiji cha Ndulamo Kata ya Iwawa Mkuu wa Kituo cha Polisi Makete Jackson Mrema amewaasa madereva hao kufuata Sheria na kutumia vifaa vinavyotakiwa wakati wote wakiwa barabaran ikiwemo viakisi mwanga.

Akikabidhi viakisi mwanga hivyo mlezi wa kikundi hicho Rabson Mahenge(Mahenge Pharmacy) amewaasa waendesha pikipiki kuwa makini katika kazi yao na kuwashauri kutunza kile wanacho kipata kwa lengo la kuwasaidia katika maisha yao huku wakilinda malengo ya kikundi.

bodaboda ndulamo wakiwa katika msafara baada ya kukabidhiwa viakisi mwanga

Afande Daurat Jabir kutoka kitengo cha Usalama barabarani Wilaya ya Makete amesema kuna umuhimu mkubwa wa waendesha pikipiki kuvaa viakisi mwanga kwa sababu itawasaidia kujulikana kwa uraisi na itawasaidia kuonekana wakati wa usiku lakini ni kifaa muhimu katika kazi ya usafirishaji wa abiria pamoja na kuvaa kofia ngumu.

Baadhi ya madereva wa pikipiki akiwemo Micklad Mahenge, Omari Mahenge na Yodam Mahenge wamemshukuru mlezi wa kikundi cha bodaboda Ndulamo kwa kuendelea kuwaunga mkono na kushirikiana katika mambo mbalimbali na wameahidi kuwa makini na kufuata sheria za usalama barabarani wakati wote