Kitulo FM

Maafisa ugani watakiwa kusimamia zao la ngano Makete

April 17, 2024, 6:24 am

picha ya zao la ngano ikiwa shambani picha na mwandishi wetu

katika kusimamia na kutekeleza kwa vitendo mpango wa Serikali wa kufungua fulsa za kiuchumi katika Wilaya ya Makete maafisa ugani wametakiwa kusimamia kilimo cha zao la ngano kwalengo la kuleta tija kiuchumi kwa wananchi wa Wilaya ya Makete.

Na Aldo Sanga

Mkuu wa wilaya ya makete Mh:Juma Sweda amewataka maafisa ugani kusimamia ipasavyo utekelazaji wa kilimo cha zao la ngano ili kufikia malengo na kuleta tija kwa wananchi wa makete katika kuinua uchumi.

Dc Sweda akiwa kwenye kikao kazi na timu ya wataalamu kutoka ofisi ya mkurugenzi Makete picha na Aldo Sanga

Mh:Juma Sweda amewaagiza maafisa ugani kusimamia wakulima wote waliochukua mbegu ya ngano kwaajili ya kupanda huku akiwataka kutoa taarifa ya maendeleo ya zao hilo kila wakati ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa ukuaji wa ngano.
Itakumbukwa kuwa Serikali imetoa jumla ya tani 500 za ngano ikiwa na lango la kufanya zao hilo kuwa nizao la kimkakati lililolenga kumwinua mwananchi wa Makete kiuchumi na kua wazalishaji wa ngano katika taifa la Tanzani .

sauti ya DC Sweda akiongea na maafisa ugani Makete

Kwa upandewake mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Makete Williamu Makufwe amewataka maafisa ugani kuwa watatuzi wa changamoto za wakulima badala ya kuibua changamoto zisizo na tija kwa manuufaa ya wakulima na wanamakete kwa ujumla.

Ded Makufwe akizungumza na wataalamu wa kilimo
sauti ya Ded Makufwe

Baadhi ya maafisa ugani wameeleza baadhi ya changomoto zinazowakabili kuwa nipamoja na ,wakulima kutokuwa na mitaji,kilimo cha mazoeya,bei ya soko kuwa chini,mfumo wa malipo ambapo kwasasa mnunuzi anatumia mfumo wa malipo yasiyo ya keshi jambo ambalo limekua na mwitikio hasi kwa wakulima.

afisa ugani akieleza changamoto

kwa upande wa bodi na nafaka na mazao mchanganyiko CPB wameeleza umuhimu wa zao la ngano na jinsi litakavoweza kuwainua wananchi wa Makete huku wakijipanga juu ya kuhakiki ubora wa zao hilo ili kukidhi soko la dunia.

Afisa ubora kutoka CPB Iringa Bi,Judith Kaoneka akizungumzia mpango wa CPB katika kuhakiki ubor wa zao la ngano
afisa ubora toka CPB Iringa Bi,Judith Kaoneka