Kitulo FM

Bodaboda Ndulamo wakusanya Milioni 16 kwa mwaka

November 28, 2023, 11:58 am

baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na jeshi la polisi kwenye mkutano na waendesha bodaboda.picha na mwandishi wetu

licha ya jitihada za serikali kuendelea kutoa elimu kwa vijana kuanzisha vikundi pamoja na kupata mikopo vijana wa bodaboda ndulamo kupitia kikundi chao wameweza kukusanya shilingi milioni 16 kwa miaka miwili ambazo zimekuwa zikiwasidia katika kutatua changamoto zao

na mwandishi wetu

Zaidi ya sh milioni 16 zimekusanywa kwa muda wa mwaka mmoja  na wanachama 50 wa kikundi cha wasafirishaji wanaotumia pikipiki maarufu kama bodaboda katika kijiji cha Ndulamo kilichopo kata ya Iwawa

Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa kikundi hicho katika ofiisi za kijiji cha Ndulamo  mwenyekiti Bw Festo mahenge amesema lengo la kuanzisha kikundi hicho ni kusaidiana katika matatizo na furaha pamoja na kukopeshana ili kikundi kiweze kukua na wameweka utaratibu mzuri wa namna ya kusimamia na kuendesha umoja huo ili uweze kuwasaidia wanakakikundi wote katika kujikwamua kiuchumi

mwenyekiti wa kikundi Bw Festo mahenge
baadhi ya waendesha pikipiki maarufu bodaboda kijiji cha ndulamo katika picha ya pamoja

Kwaniaba ya mlezi wa kikundi hicho ambaye ni Rabson Mahenge {Mahenge Phamarcy }aliyewakilishwa na Bw Majuto Mbwilo anewapongeza wanakikundi kwa kuendeleza umoja huo kwani kitawasaidia kutatua changamoto mbalimbali  na kuwaasa kutumia vizuri fedha walizopata leo kwa ajili ya familia na kuwakabidhi sh laki  tano {500000} kwa ajili ya kuendeleza kikundi hicho

mlezi wa kikundi Rabson Mahenge

PC Daulath  Jabir kutoka kitengo cha usalama barabarani amewaasa wanakikundi hao  kua na leseni na kuacha kuendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu { helment  }kwani hili linahatarisha maish yao na abiria huku akiwataka kufuata sheeria za usalama barabarni ikiwemo kuzingatia alama za barabarani, , kutoendesha mwendoka na kutotumia kilevi

PC Daulath  Jabir kutoka kitengo cha usalama barabarani

PC Daulath  Jabir kutoka kitengo cha usalama barabarani makete

Kwaupande wake mtendaji wa kijiji cha Ndulamo Bi Mariam Cherehani amesema amefarijika sana kuona wameungana kwa ajili ya kusaidiana amewaasa wameendelee kushirikiana na kutoa taarifa  ili kutokomeza wizi kwani bodaboda ndiyo wanatuhumiwa kusafirisha vitu vinakua vimeibwa

 mtendaji wa kijiji cha Ndulamo Bi Mariam Cherehani

Askali akitoa elimu kwa waendesha pikipiki ndulamo

Makam mwenyekiti wa muungano kijiji cha Ndulamo immanuel amesema kazi ya bodaboda inachangamoto nyingi ikiwemo kuporwa pikipiki na ajari jambo pekee litakalowasaidia ni kudumisha umoja huku akiwataka kuendelea kuzingatia usafi ili kuwavutia wateja

Makam mwenyekiti wa muungano kijiji cha Ndulamo immanuel

Kikundi cha waendesha pikipiki ndulamo kinawanachama zaid ya 50 na kimetimiza miaka miwili huku kikijidhatiti kusaidiana na kukumbusha sheria za usalama barabara kwa wanachama wake ili kupungiuza ajari za barabarani