Kitulo FM

DED Makete akutana na wadau wa elimu

February 13, 2024, 8:06 am

Ded Makufwe kati akitoa tathimini ya ufaulu katika shule za msingi na sekondari .picha na Lulu Mbwaga

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe Amewataka wadau wa Elimu ikiwemo walimu maafisa elimu kusimamia kikamilifu taaluma katika wilaya ya Makete ili kuinua kiwango cha taaluma Makete.

Na Lulu Mbwaga

Mkurugenzi Mtendaji halmashaur ya Wilaya Makete Ndg William Makufwe ameongoza kikaoo Cha upimaji na tathmini ya utendaji kazi wa wa huduma ya elimu kwa waratibu wa elimu ngazi ya kata ,wakuu wa shule za sekondar na msingi pamoja na maafisa elimu ngazi ya Wilaya, mdhibiti ubora na chama Cha walimu Wilaya ya Makete lengo ni kuweka mikakati ya namna ya kuongeza ufaulu

Kikao hicho kimefanyika tarehe 12/2/2024 katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Iwawa iliyopo kata ya Iwawa ,Wilaya ya Makete ambapo Ndg Makufwe amesema viongozi hao wajitathmin utendaji kazi wao wa utoaji elimu kwani jukumu lao kubwa ni kusimamia na kumfuatilia taaluma mashuleni hivyo kwa sasa wahakikishe halmashaur ya Wilaya ya Makete inaomgeza ufaulu kwa wanafunzi

Ameongeza kua halmashaur itaitisha kikao Cha wadau wa elimu Wilaya ya Makete ambacho kitakua na uwakilishi wa makundi mbalimbali Ili kua na mkadala mpana wa namna ya kuboresha elimu huku akiwataka wasimamizi wa elimu kutimiza majukumu Yao kwani Kuna baadhi ya changamoto ambazo zimepelekea kutokua na ufaulu mzuri zilizosababishwa na kukosa usimamiz mzuri kutoka kwa waratibu wa elimu na wakuu wa shule

Kwa upande wake afisa elimu taaluma kutoka idara ya elimu awali na msingi Ndg Bakari Msuya amesema wameweka mikakati mbalimbali ya kukuza na kuongeza ufaulu ikiwemo kuhakikisha madarasa ya mitihani wanasoma kwa muda wa ziada, kufanya ukaguzi wa ndani wa shule kwa kutumia kamati za udhibiti ubora wa shule na kumfuatilia kwa kina kila mwanafunzi anamudu vyema kusoma na kuandika

Kikao hicho kwa pamoja wakatoka na maadhimio mbalimbali ikiwemo viongozi hao wa elimu ngazi ya kata kuitisha kikao kila mwezi kwa ajili ya kujadili maendeleo na changamoto za wanafunzi na namna ya kukabiliana nazo kwa wananfunzi wa madarasa ya mitihani na kila Mwalimu Mkuu na Mkuu wa shule awe na mkataba na Mwalimu ambao utaonyesha makubaliano ya utendaji kazi wake