Kitulo FM

Wahitim 34 watunukiwa vyeti shule ya sekondari Kitulo

October 7, 2023, 9:31 am

Wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari kitulo picha na Aldo sanga

Kuelekea mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya sekondari jumla ya wanafunzai 34 wametunukiwa vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Kitulo iliyopo Makete Njombe

na Aldo Sanga

Jumla ya wanafunzi 34 wa metunukiwa cheti cha kuhitim masomo ya kidato cha nne katika maafari ya 12 katika shule ya sekondari kitulo,

Akikabidhi vyeti vya kuhitim elimu ya sekondari Mh:Abeli Mahenge diwani wa kata ya kitulo ambaye ndiye alikua mgeni rasmi amewapongeza vijana hao kwa kuvumilia katika masomo yao huku akiwataka kutia nia katika kuyafikia malengo yao

Mh:Mahenge ameongeza kua chanagamoto zilizoelezwa hasa katika kuboresha na kuongeza miundombinu ya shule hususani katika majengo Halmashauli ya Wilaya kupitia mpango wa maendeleo TASAF Imetoa fedha na tayari ujenzi wa bweni umeshafikia hatua za umaliziaji hata hivyo ameahidi kuziwasilisha katika ngazi husika

sauti ya Mh:Abeli Mahenge diwani wa kata ya kitulo (mgeni rasmi)

Mwl, Degdus Ezekiel Mwatujelele ni makam mkuu wa  shule ya sekondari kitulo kwaniaba ya mkuu wa shule ameeleza mafanikio ya shule kua nipamoja na ongezeko wa ufaulu katika shule ambapo katika mitihani ya kujipima baadhi ya wanafunzi walifanya vizuri mwanafunzi mmoja kutoka shule ya kitulo alishika nafasi ya kwanza na wapili nafasi ya tatu kiwilaya katika matokeo ya kidato cha pili huku akiongeza kua mafanikio hayo yametokana na ushirikiano wa walimu serikali pamoja na wazazi,

sauti ya Mwl:Degdus Ezekiel Mwatujelele ni makam mkuu wa  shule ya sekondari kitulo

Shule ya sekondari kitulo nimiongoni mwa shule zilizopo katika wilaya ya Makete karibu na hifadhi ya Taifa ya kitulo  yenye jumla ya wanafunzi 186 hadi sasa imesha fanya maafari 12 tangu kuanzishwa kwake.

mgeni rasmi akizungumza na wananchi kwenye maafari ya 12 kitulo sekondari picha na Aldo sanga