Kitulo FM
Kitulo FM
5 August 2026, 2:55 pm

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Chrispin Francis Chalamila
Ofisi ya Takukuru imeishukuru serikali kwa kutoa fedha za kuhakikisha wanapata jengo la Takukuru makete kutokana na kutumia majengo ambayo hayajakidhi viwango
na mwandishi wetu
Jengo jipya la ofisi ya Takukuru wilaya ya makete mkoani Njombelililopo Mtaa wa Dombwela karibu na Makao Makuu ya Wilaya ya Makete limezinduliwa hii agasti 4,2026 na mkurugenzi mkuu wa takukuru Taifa ndg Chrispin Chalamila
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mgeni Rasmi ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Chrispin Francis Chalamila, ndg chalamila amewasihi watumishi wa Takukuru wilaya ya makete kuendelea kulitunza jengo hilo ili liweze kudumu kwa kizazi cha sasa na kijacho huku akiwataka wananchi kulitumia jengo hilo katika kutoa taarifa za kweli za rushwa ili ziweze kushughulikiwa
sauti ya mkurugenzi mkuu 01

muonekano wa jengo jipya ofisi ya Takukukuru Makate
Aidha ndg Chalamila amemshukuru mhe Samia Suluhu Hassani kwa kuendelea kuiwezesha Takukuru kwa rasilimali watu, vitendea kazi pamoja na fedha ili kuweza kurahisisha utendaji kazi ulio bora pamoja na utoaji wa elimu ya rushwa kwa wananchi
sauti ya chalamila 02
Mkurugenzi wa usimamizi wa milki ya Takukuru muhandisi ndg Emanuel kiagwa akisoma taarifa ya mradi wa jengo hilo mbele ya mkurugenzi mkuu wa Takukuru amesema kuwa jengo hilo mpaka kukamilika kwake limeghalimu zaidi ya shilingi milioni 416.9
sauti ya emanuel 03

mkuu wa wilaya ya makete mhe kissa Kaswongwa akizungumza kwenye uzinduzi huo
Nae mkuu wa mkoa wa Njombe mhe Antoni Mtaka amemweleza mkurugenzi mkuu wa Takukuru kuwa ni wakati pia wakuweza kuwatumia wakandarasi wazama katika kutekeleza miradi mbali mbali hapa nchini
sauti ya mkuu wa mkoa mhe Mtaka 04
Mkuu wa wilaya ya makete mhe Kissa Kasongwa pamoja na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya makete ndg Clemence Ngajilo wamesema kuwa kupitia Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na mhe Samia Suluhu Hassani imefanya mageuzi makubwa katika wilaya ya makete kwa utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa manufaa ya wananchi
sauti ya dc vs mwenyekiti ccm 05

wanafunzi, wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa jengo la Takukuru
Akizungumza mwenyekiti mstaafu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe ndg Jasel Mwamala amesema kuwa viongozi wa mila wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha amani inatawala katika wilaya ya makete huku akisisitiza jengo hilo lililozinduliwa hii leo likawe chachu kwao katika utendaji kazi wao wa kuzia na kupamba na rushwa
sauti ya mwamala 06
Hafla ya uzinduzi huo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, watendaji wa taasisi tofauti pamoja na wananchi.